Jumanne 12 Mei 2026 - 16:39
Waislamu na watu huru duniani waiunge mkono Hizbullah ya Lebanon

hawza/ Ayatullah Hussein Nouri Hamedani, huku akilaani mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni muuaji wa watoto dhidi ya Lebanon, amewataka Waislamu wote na watu huru duniani kuiunga mkono Hizbullah ya Lebanon.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Nouri Hamedani, huku akilaani mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni muuaji wa watoto dhidi ya Lebanon, alisisitiza: Ni lazima Waislamu wote na watu huru duniani wasimame kwa msimamo madhubuti dhidi ya uvamizi na jinai hizi, walaani mashambulizi haya, na watangaze kuwaunga mkono wananchi wa Lebanon hususan Hizbullah kipenzi, ambayo iko mstari wa mbele kwa ustahimilivu na ushujaa katika kutetea nchi na wananchi wa Lebanon.

Matini ya ujumbe wake ni kama ifuatavyo:

بسم الله الرحمن الرحیم

Mashambulizi makubwa ya utawala wa Kizayuni nchini Lebanon, ambayo ni dhihirisho la tabia ya kinyama ya utawala huu dhalimu na muuaji wa watoto, yamesababisha huzuni na masikitiko makubwa.

Jinai hii inafanyika kwa uungwaji mkono wa moja kwa moja na serikali ya kigaidi ya Marekani, pamoja na ukimya wa baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu, na vilevile wale wanaodai kwa uongo kutetea haki za binadamu.

Ni lazima Waislamu wote na watu huru duniani wasimame kwa misimamo madhubuti mbele ya uvamizi na jinai hizi na wayalaani mashambulizi haya, pamoja na kutangaza uungaji mkono wao wa kila upande kwa wananchi wa Lebanon, hususan Hizbullah kipenzi, ambayo iko katika njia ya kuitetea nchi na wananchi wa Lebanon kwa ustahimilivu na ushujaa.

Hussein Nouri Hamedani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha